Msanii nguli kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amezindua zoezi la kuwasajili wasanii ambao wanatamani kujiunga na chama chake cha Uganda Musicians Federation.
Ni Zoezi ambalo litaandeshwa na timu ya wataalam wa masuala ya muziki nchini Uganda ambao watawachagua wasanii kutoka maeneo mbali mbali nchini Uganda.
Ikumbukwe chama cha Uganda Musician Federation lilizunduliwa na Mwanamuziki Jose Chameleone mwezi juni mwaka huu.
Lengo kuu la kuanzishwa kwa chama hicho lilikuwa ni kuangazia maslahi ya wasanii nchini uganda ambao wamekuwa wakisuasua kimuziki.
Chameleone aliweza kuwasajili wasanii kama Pallaso, Weasel, Feffe Buusi na wengine wengi. Chini ya mwongozo wake, walipata fursa ya kukutana na Jenerali Salim Saleh kutafuta msaada wa kifedha lakini wachache wao walipewa pesa taslimu.
Wanamuziki waliokosa pesa hizo walihamua kumkimbia chameleone jambo lilomlazimu bosi huyo wa Leone island kuchukua mapumziko mafupi.