You are currently viewing CHAMELEONE: KOLABO ZA KIMATAIFA HAZINA MAANA KWA WASANII CHIPUKIZI

CHAMELEONE: KOLABO ZA KIMATAIFA HAZINA MAANA KWA WASANII CHIPUKIZI

Lejendari wa muziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amedai kwamba kufanya kolabo na mastaa wa kubwa duniani haina faida yeyote kwa msanii.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Chameleone amesema haamini katika suala la kufanya kolabo na wasanii wakubwa duniani ili kupenya kwenye soko la kimataifa.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Forever” amesema kolabo hizo hazina maana kwa sababu mastaa hao hushindwa kuitangaza kolabo zenyewe kwenye nchini zao na badala yake mzigo wa kuitangaza project husika ubaki upande mmoja.

Chameleone ni moja kati ya wasanii nchini uganda waliofanya kazi ya pamoja na mastaa kubwa duniani kama vile Beenie Man, Davido, Sizzla,Koffi Olomide na wengine wengi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke