Kufuatia mashtaka ya unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wadogo na makosa mengine yanayomkabili nguli wa muziki wa R&B duniani, R. Kelly, mtandao wa Youtube umechukua hatua ya kuzifungia channel rasmi za staa huyo.
Channel hizo ni pamoja na R Kelly TV na R Kelly Vevo ila, nyimbo za nguli huyo bado zipo Youtube kupitia channel za watu wengine.
Kwa sasa R.Kelly anasubiria hukumu yake ambayo imetajwa kutolewa Mei 4 mwakani, na huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 au kifungo cha maisha gerezani.
|