Staa wa muziki kutoka Konde Gang Cheed ametangaza kuachia EP yake ya kwanza tangu ajiunge na lebo hiyo ya muziki inayomilikiwa na Harmonize.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Cheed ameachia swali kwa mashabiki zake kama wapo tayari kuipokea EP yake mpya inayosomokea “Are you ready for my first Extended Playlist?! Stay ready!! 🚨#Cheed #Kondegang4you”
Pamoja na kutoa taarifa hiyo, Cheed hajaweka wazi jina la EP hiyo pamoja na tarehe ya kuachia EP yenyewe.
Cheed atakuwa msanii wa pili kuachia ndani ya mwaka huu baada ya Killy ambaye aliwabariki mashabiki zake za Green light EP yenye jumla ya nyimbo 5 za moto.