Wasanii Cheed na Killy huenda kwa sasa wakawa hawataki kuona chochote kuhusu Harmonize.
Wawili hao wameamua kumu-unfollow bosi wao huyo wa zamani katika kurasa zao za Instagram baada ya lebo ya Konde Music Worldwide kusitisha mkataba wao kwa sababu ambazo hawakuziweka wazi.
Utakumbuka mwisho mwa wiki iliyopita, Cheed na Killy waliwasilisha lalama zao kwa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kupata mwanga kuhusu sakata la kutimuliwa kwao.
Lakini kikao cha kutatua mgogoro wao na lebo hiyo hakikuweza kufanyika baada ya uongozi wa Konde Music Worldwide kushindwa kufika Basata.