Rapa kutoka nchini Tanzania Chidi Benz amewapa mashabiki wake orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya ya “Wa2 Wangu” anayoitarajia kuitoa hivi karibuni.
Chid benz ambaye ni mshindi mara nne wa Kill Music Awards kupitia tuzo ya msanii Bora wa Hip Hop nchini tanzania, ameorodhesha jumla ya nyimbo 18 kutoka kwenye album hiyo, huku ikiwa na collabo 5 pekee,ambapo amewapa mashavu wasanii kama Badest 47, Brian Simba kusikika kwenye album hiyo.
Hata hivyo, Chidi tayari ameshaachia nyimbo 6 kutoka kwenye album hiyo, ambazo ni Nahamia Bar, Jirani, Walete, One, King of the Jungle na Hilo Ngoma.
Ikumbukwe kuwa, hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwa mtu mzima Chidi Beenz baada ya Dar Es Salaam Stand Up ya mwaka wa 2010