Album mpya ya rapa Chidi Beenz iitwayo WA2 WANGU imetoka rasmi na sasa inapatikana kupitia majukwaa mbalimbali ya ku-stream muziki mtandaoni.
Album ya WA2 WANGU yenye jumla ya nyimbo 18, ina kolabo 5 pekee, Chidi akiwapa mashavu wasanii kama Baddest, Brian Simba na wengineo kusikika kwenye album hiyo.
Hata hivyo, Chidi tayari alishaachia nyimbo 6 toka kwenye album hiyo, ambazo ni Nahamia Bar, Jirani, Walete, One, King of the Jungle na Hilo Ngoma.
Rapa Chidi Beenz ambaye ni mshindi mara nne Kill Music Awards kupitia tuzo ya msanii Bora wa Hip Hop nchini Tanzania, album yake hii mpya (Wa2 Wangu) inaifuata album ya “Dsm Stand Up” ambayo ndio album yake ya kwanza kuiachia kwenye muziki wake, ilitoka mwaka 2010.