You are currently viewing Chifu wa Kuna Kuna John Ogilo alamba shavu la ubalozi Huduma Center Kisumu

Chifu wa Kuna Kuna John Ogilo alamba shavu la ubalozi Huduma Center Kisumu

Chifu wa miondoko ya kisasa nchini John Ogilo Migun, ameingia ubia wa kufanya kazi na Huduma Center Kenya mjini Kisumu ambapo anatarajiwa kutumia ushawishi wake kusakata densi kutangaza huduma za taasisi hiyo.

Kulingana na video iliyochapishwa na Kituo cha Huduma cha Kisumu kwenye mitandao yake ya kijamii, Bwana Ogilo, amesikika akitoa wito kwa umma hasa vijana kutumia fursa ya kuongezwa kwa muda wa kazi katika kituo hicho kupata huduma za serikali.

““Sasa watu nguyaz, mabazuu, mayutman, services sasa ni saa moja asubuhi mpaka saa moja jioni. Unatoka job, unatoka colle, unatoka works unaingia Huduma center,” Alisema John Ogilo

Ikumbukwe John Ogilo mwenye umri wa miaka 38 ambaye ni naibu chifu wa eneo la Kisumu ya kati alipata umaarufu nchini kupitia wimbo wa “Kuna Kuna” wa wasanii Vic West, Brandy Maina, Fathermoh, Savara na Thee Exit Band.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke