You are currently viewing CHIKE AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA JUU YA TUHUMA ZA KUTUMBUIZA WIMBO WA RADIO & WEASEL BILA IDHINI

CHIKE AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA JUU YA TUHUMA ZA KUTUMBUIZA WIMBO WA RADIO & WEASEL BILA IDHINI

Mwanamuziki kutoka Nigeria Chike amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya msanii Weasel Manizo kumchana kwa hatua ya kuimba wimbo wa Radio na Weasel uitwao “Breath Away” kwenye moja ya performance yake wiki iliyopita.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Chike amesema hakuwa na nia ya kumvunjia heshima Weasel au mtu yeyote ila alikuwa ni njia ya kutoa heshima zake kwa marehemu Mozey Radio ambaye alikuwa mmoja kati ya wasanii  walioacha alama kwenye muziki wa Afrika.

Hata hivyo chanzo cha karibu na Weasel kimesema msanii huyo ana mpango wa kuelekea mahakamani kuwafungulia mashtaka waandaji wa show yChike kwa hatua ya kumruhusu msanii huyo wa Nigeria kutumbuiza wimbo wa Radio & Weseal bila ridhaa yao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke