You are currently viewing CHIKI KURUKA AMKINGIA KIFUA BIEN WA SAUTI SOL KWA MADAI YA KUPANGA UZAZI

CHIKI KURUKA AMKINGIA KIFUA BIEN WA SAUTI SOL KWA MADAI YA KUPANGA UZAZI

Mke wa msanii Bien, Chiki Kuruka amemkingia kifua msanii huyo kutokana na kauli yake ya kutaka kumsaidia kupanga uzazi kwa kukata mshipa wake wa uzazi maarufu vesectomy.

Akizungumza na Mpasho mrembo huyo amesema kauli hiyo ilitafsiriwa vibaya na waandishi wa habari kwani Bien alikuwa anajaribu kuwaelimisha wanaume kuhusu umuhimu wa kuwasaidia wake zao kwenye suala la kupanga uzazi.

Katika hatua nyingine amekosoa vyombo vya habari kwa kuripoti habari za uwongo dhidi ya mume wake Bien huku akisisitiza haja ya waandishi kuwa mstari wa mbele katika kuzingatia maadili ya uandishi wa habari ikiwemo kuandika habari za ukweli na uhakika kama njia ya kuepusha upotoshaji.

Utakumbuka mwezi Julai mwaka huu Bein alinukuliwa akisema yupo tayari kukata mshipa wa uzazi maarufu vasectomy punde atakapo pata watoto na mke wake Chiki Kuruka.

Msanii huyo wa Sauti Sol ameenda mbali Zaidi na kusema kwamba upangaji uzazi barani Afrika ni swala ambalo limeachiwa wanawake, hivyo hawezi kumwachia mke wake mzigo huo pekee licha ya wanaume wengi kuogopa kufanyiwa vasectomy.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke