Mkali wa muziki nchini Chikuzee ametusanua kuwa album yake mpya imekamilika.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “In Love” ameweka wazi hilo kwenye moja ya Interview sambamba na kuwapa challange mashabiki wake kupendekeza jina kali ambalo atalitumia kwenye album hiyo.
Hata hivyo Chikuzee hajatuambia idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album hiyo wala tarehe rasmi ya album yenyewe itaingia sokoni ila amesema ataachia ngoma tatu kutoka kwenye album hiyo hivi karibuni.
Kwa hiyo mashabiki wa msanii huyo mkae mkao wa kuipokea album yake mpya itakayoingia sokoni hivi karibuni