You are currently viewing CHIMANO WA SAUTI SOL AKIRI KUWA MPENZI WA JINSIA MOJA

CHIMANO WA SAUTI SOL AKIRI KUWA MPENZI WA JINSIA MOJA

Mwimbaji maarufu wa muziki wa Afro pop nchini Chimano amejitokeza hadharani na kudai kuwa yeye ni mpenzi wa jinsia moja.

Chimano ambaye ni mmoja wa waimbaji maarufu wa kundi la Sauti Sol amejitokeza kama mpenzi wa jinsia moja alipokuwa akielezea wimbo wake mpya, wa Friday Feeling, ambao amewashirikisha jamii ya LGBTQ.

“Hakuna kujificha tena,” ameambia vyombo vya habari vya ndani nchini Kenya.

Msanii huyo amesema kwa sasa anaishi ukweli wake na atatumia muziki wake kupinga taasubi za kiume zenye sumu, chuki na unafiki.

Tamko hilo la hadharani linaweza kupiga jeki juhudi za kupigania haki za watu wa jamii ya LGBTQ nchini Kenya, ambapo mapenzi ya jinsia moja ni haramu na ukipatikana na hatia unafungwa hadi miaka 14 jela.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke