You are currently viewing CHOSEN BECKY AKERWA NA WANAOSHINIKIZA WASANII WAPROMOTI KAZI ZA WENZAO

CHOSEN BECKY AKERWA NA WANAOSHINIKIZA WASANII WAPROMOTI KAZI ZA WENZAO

Msanii Chosen Becky amewataka wasaani kutowapa shinikizo wenzao  kuchapisha matangazo ya shows kwenye mitandao ya kijamii.

Hii ni baada ya DJ Nimrod kuzua gumzo mtandaoni kwa kusema kuwa Juliana Kanyamozi hakupaswa kupewa support kutoka kwa wasanii wengine kwa sababu huwa hawaungi mkono wasanii wengine kwenye shughuli zao.

Sasa Chosen Becky aliamua kumkingia kifua juliana kanyamozi kwa kusema kuwa sio vibaya wasanii kushirikiana kwenye kazi zao ila hawapaswi kulazimishwa kuposti shows za wasanii wengine ila wafanya hivyo kwa hiari yao.

Hitmaker huyo wa “Wano” amesema kuna shows nyingi ambazo zinafanyika kila siku na msanii akiamua kuzipoati kila siku akaunti yake ya mitandao ya kijamii itageuka kuwa runinga ya matangazo ya biashara.

“It is good to support one another but it’s not a must to post every poster of a musician holding a concert. I don’t think that’s good. We need to be allowed to choose those to support. If I post about B2C, another can post about Fameika…like that,” Alisema Chosen Becky .

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke