Msanii kutoka nchini Uganda Chozen Blood amefunguka sababu za ukimya wake kwenye muziki wake.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Chozen Blood amesema karibu ajitoe uhai kipindi cha Corona baada ya muziki wake kukosa kumuingizia kipato licha ya kuwekeza pesa nyingi.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sharp Shooter” amesema alifulia kiuchumi kiasi cha kushindwa kujikimu kimaisha jambo ambalo amedai lilimfanya kupata na msongo wa mawazo.
Msanii huyo wa zamani wa lebo Team No Sleep amesema kwa sasa ameanza kupata nafuu na tayari amerudi tena studio kwa ajili ya kuendelea na harakati za kurekodi muziki wake.
Chozen Blood alipata umaarudu nchini Uganda mwongo mmoja uliopita kupitia singo yake iitwayo Pressure ya Love aliyomshirikisha Walden.
Kwa sasa anafanya vizuri na Album yake iitwayo “1am Chozen” ambayo iliingia sokoni mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya ngoma 11 za moto.