Nyota wa Pop na RnB kutoka Marekani, msanii Chris Brown tayari ameachia album yake mpya iitwayo “Breezy” yenye jumla ya ngoma 24.
Album hii mpya inakuwa ni album ya 10 kwa Chris Brown ikiifuata Indigo iliyotoka mwaka 2019.
“Breezy” imewashirikisha wasanii kama Wizkid, Ella Mai, H.E.R., Lil Wayne, Blxst, Anderson .Paak, Jack Harlow, Tory Lanez na wengine.