You are currently viewing CHRIS BROWN ABURUZWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

CHRIS BROWN ABURUZWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

Mwanamuziki wa RnB kutoka Marekani Chris Brown amefunguliwa mashtaka ya ubakaji na mwanamke mmoja ambaye hakutaka jina lake lifahamike.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Disemba 30, mwaka 2020 kwenye boti iliyokuwa imepaki nje ya nyumba ya Diddy mjini Miami ambapo kulikuwa na party.

Chris Brown anadaiwa kuwa alimualika mwanamke huyo kuja kwenye party kwa kupitia rafiki yake, na baada ya kuwasili, Breezy alianza kumtongoza na kumuuliza kama anataka kinywaji. Alienda jikoni na kumpatia mwanamke huyo kikombe chekundu kikiwa na kinywaji ambacho kimechanganywa na dawa za Kulevya.

Baada ya kunywa kinywaji kile, mwanamke huyo alianza kuhisi kuishiwa nguvu na usingizi, ambapo Chris Brown alimtupa kitandani na kuanza kumbaka.

Kwenye shtaka hilo mwanamke huyo anadai ($20 million) zaidi ya shillingi billioni 2.3 za Kenya kama fidia kwa matatizo ambayo Chris Brown amemsababishia ikiwemo mfadhaiko wa kihisia.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke