Mwanamuziki nyota kutoka Marekani Chris Brown kwenye mahojiano na Drink Champs ameweka wazi kwamba rapa mkongwe Diddy alikataa kumsaini kwenye Label yake ya “Bad Boy”, kipindi ambacho alikuwa na umri wa miaka 12.
Breezy amesema kwa kipindi kile miaka ya 1993 na kuendelea, record label kubwa ilikua ya rapa Diddy, hivyo kukataliwa kwake hakukuweza kumkatisha tamaa kufikia ndoto zake.
Chris brown kwa sasa yupo kwenye media tour kwa ajili kutangaza album yake mpya “Breezy”, pamoja na ziara yake ya muziki ambayo itazunguka kwenye miji 27 ya Kaskazini mwa Marekani, itaanza Julai 15 mwaka huu.