Staa wa muziki kutoka nchini Marekani Chris Brown ameripotiwa kuwa amepata mtoto wa tatu na mrembo mwanamitindo aitwaye Diamond Brown ambaye ame-share taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram.
Mrembo huyo pia amelitaja jina la mtoto huyo wa Kike kuwa ni Lovely Symphani Brown. Jina la katikati la mtoto ‘Symphani’ limepelekea watu kuhisi Breezy ndio Baba wa mtoto huyo, kwani limefanana na jina la taasisi yake iitwayo Symphonic Love.
Chris Brown tayari ana watoto wawili; Aeko Catori Brown mwenye umri wa miaka miwili, pia ana binti mkubwa Royalty mwenye umri wa miaka 8.