You are currently viewing CHRIS BROWN AMPONGEZA RIHANNA NA MPENZI WAKE ASAP ROCKY KWA KUPATA MTOTO WA KIUME

CHRIS BROWN AMPONGEZA RIHANNA NA MPENZI WAKE ASAP ROCKY KWA KUPATA MTOTO WA KIUME

Moyo wa Chris Brown bado upo kwa Rihanna, hii ni baada ya kumpongeza Ex wake huyo kwa kupata mtoto wa Kiume pamoja na mpenzi wake Asap Rocky.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Breezy ameandika ujumbe unaosomeka “Congratulations,” akiambatanisha na emoji za kushukuru huku pia akisindikiza na emoji ya mama mjamzito.

Rihanna ambaye amejifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume akiwa na umri wa miaka 34, Mei 13 mwaka huu, ripoti mbalimbali zinaeleza kwamba mtoto wake anaendelea vizuri ijapokuwa jina la mtoto huyo halijawekwa wazi.

Mwaka 2009 Chris Brown alimpiga mwanadada Rihanna wakiwa kwenye gari na kumsababishia michubuko usoni kiasi cha kupelekea wawili hao kuvunja uhusiano wao wa kimapenzi.

Hata hivyo Breezy alihukumiwa kifungo cha nje miaka 5 huku akiwa chini ya uangalizi pamoja na kufanya kazi za Kijamii.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke