Chris Brown amemuunga mkono mcheza Kikapu Kyrie Irving ambaye amegoma kuchanjwa chanjo ya COVID-19.
Kupitia Insta Stories yake kwenye mtandao wa Instagram Chris Brown amesema ana simama na nyota huyo wa Brooklyn Nets na kumuita shujaa wa ukweli.
Kyrie Irving anaendelea kuvigusa vichwa vya habari duniani kwa kuigomea chanjo ya COVID-19 ambayo imefanywa kuwa lazima kwa wana michezo wote, hivyo kuweka hatiani mustakabali wake wa kucheza kwenye ligi hiyo hasa michezo ya nyumbani kwa sheria za Jiji la New York.
Staa huyo ameitaja sababu ya kugoma kuchanjwa, akisema kuwa mtu hapaswi kulazimishwa kufanya jambo lolote kwenye mwili wake, na anasimama na wote ambao wanaamini kipi ni sahihi.