Staa wa muziki nchini Marekani, Christopher Maurice Brown maarufu Chris Brown ametangaza ujio wa kazi zake mpya mwakani.
Kupitia Insta Story kwenye mtandao wa Instagram Chris Brown ameandika ‘BREEZY ERA STARTS IN JANUARY’, ujumbe uliotafsiriwa kama tangazo la ujio wa album yake ya 10 ya Breezy ambayo inadaiwa kuwa itatoka Januari mwaka wa 2022.
Album hiyo ya Brown iliyosubiriwa kwa muda sasa inatarajiwa kuwa itatoka ikiambatana na filamu fupi.
Album ya mwisho kutoka kwa mtu mzima Chris Brown ilikuwa ni Indigo iliyotoka mwaka wa 2019 ikiwa na nyimbo zilizofanya vizuri ambazo ni pamoja na ‘Back To Love’ na ‘No Guidance’ ft. Drake.