You are currently viewing CHRIS BROWN AZIMWAGA SIFA KWA WIZKID

CHRIS BROWN AZIMWAGA SIFA KWA WIZKID

Staa wa muziki nchini Marekani Chris Brown ameshindwa kuficha furaha yake kwa heshima ambayo alipewa na Wizkid usiku wa kuamkia Novemba 29  kwa kupandishwa kwenye Jukwaa la ziara ya ‘Made In Lagos’ ambapo kiliwaka kwenye ukumbi wa 02 Arena Jijini London Uingereza.

Kupitia ukurasa wake wa instagram , Breezy amebainisha kuwa anaona ufahari kwa mafanikio ambayo ameyafikia WizKid huku akiweka wazi kuwa wana urafiki kwa zaidi ya miaka 10.

Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa wawili hao kupandishana jukwaani, Chris Brown aliwahi pia kumpandisha Wizkid jukwaani kwenye show ya Tour yake ya Amsterdam mwaka wa  2016.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke