Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Chris Brown anadaiwa kodi na mamlaka ya mapato nchini Marekani, ambapo inatajwa kuwa anadaiwa kiasi cha (USD 4 million) zaidi ya KSh. milioni 497 ambacho ni kiwango cha kodi ambayo hakulipa tangu mwaka 2022.
Mamlaka hiyo ya mapato (IRS) inamtaka Breezy alipe deni hilo haraka iwezekanavyo, nyaraka za madai hayo zinaonesha tayari serikali imeorodhesha baadhi ya mali ikiwemo nyumba na biashara zake kuwa itazichukua ikiwa atashindwa kulipa kwa muda unaofaa