You are currently viewing CHRIS BROWN MATATANI KWA KUKWEPA SHOW YAKE

CHRIS BROWN MATATANI KWA KUKWEPA SHOW YAKE

Taarifa zinanazidi kusambaa zikimuhusisha Msanii Chris brown kukimbia na pesa baada ya kughairi kutumbuiza huko Houston muda mchache baada ya kufanya Soundcheck.

The shade room imeripoti kuwa, Mwanaharakati na Mfanya biashara kutokea Houston Bi.LeJuan Bailey yupo mbioni kumchukulia Breezy hatua za Kisheria iwapo atashindwa kurejesha Mkwanja alio kimbia nao ($1.1M) ambapo March,19 Brown alitakiwa kutumbuiza katika tambasha lililoandaliwa ili kuhamasisha uchangiaji fedha kwa ajili ya wakazi ambao nyumba zao ziliharibiwa wakati wa Kimbunga Ida.

Mwanamama huyo Anasema alitimiza kila kitu ambacho CB alihitaji ikiwa ni pamoja na Kumkodishia ndege binafsi na kumpa kiasi cha Dolla za kimarekani 1.1M, lakini mzee baba baada tu ya kufanya Soundcheck likabaki vumbi lake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke