You are currently viewing CHRIS EVANS AWATAKA WALIMENGU WAMPE UHURU WA KUIKUZA PENZI LAKE NA MREMBO BRISHER KASH

CHRIS EVANS AWATAKA WALIMENGU WAMPE UHURU WA KUIKUZA PENZI LAKE NA MREMBO BRISHER KASH

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Chris Evans ametoa rai kwa mashabiki zake pamoja na vyombo vya habari kutoingilia mahusiano yake na malkia wa tiktok nchini humo Brisher Kash wakati huu penzi lao linazidi kukolea.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Chris Evans amedai kuwa kadri watu wanavyozidi kumfuatilia na kumuuliza maswali kuhusu maisha yake ya mahusiano, ndivyo wanatengeneza mazingira ya mrembo huyo kumkimbia kwani huenda akatamka maneno yanayokinzana na yale aliyomuambia kipindi wanaanza kuchumbiana.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Linda” amewataka walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wampe uhuru wa kuikuza penzi lake na Brisher Kash bila muingilio wowote.

Chris Evans na Brisher Kash wamekuwa wakionekana kwenye viwanja mbali mbali vya kukulia bata viunga mwa jiji la Kampala kwa wiki kadhaa sasa jambo ambalo limewaaminisha watu wengi kuwa huenda wawili hao wanatoka kimapenzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke