You are currently viewing CHRIS ROCK: SITAONGELEA SAKATA LA WILL SMITH  KUNIPIGA KOFI HADI NILIPWE

CHRIS ROCK: SITAONGELEA SAKATA LA WILL SMITH KUNIPIGA KOFI HADI NILIPWE

Mchekeshaji kutoka Marekani Chris Rock amesema hatozungumzia sakata la kuchapwa kofi na Will Smith hadi pale atakapolipwa pesa.

Mchekeshaji huyo alizungumza hayo mbele ya wahudhuriaji wa onesho lake juzi Ijumaa, ambapo alisema “Mimi niko sawa, nina hii show nzima, lakini sitaongelea kuhusu hilo hadi pale ambapo nitalipwa. Maisha ni mazuri, nimerudisha hali yangu ya kusikia.”

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, wameichambua kauli hiyo na kusema kwamba pengine Chris Rock anataka kulipwa pesa ndefu kwa ajili ya kufanya mahojiano maalum kuhusu tukio lile. Au pia ana mpango wa kufungua kesi dhidi ya Will Smith ambapo atalipwa pesa ndefu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke