You are currently viewing Christina Shusho aachia Tracklist ya Album yake mpya

Christina Shusho aachia Tracklist ya Album yake mpya

Mwimbaji wa nyimbo za injili Christina Shusho ameachia Tracklist ya Album yake mpya iitwayo HARARAT ambayo anatarajia kuitoa rasmi mwakani.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Shusho amebainisha kuwa Album hiyo yenye jumla ya mikwaju 25 ya moto itakuja kuwa album bora Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla kulingana na ubora wa maandalizi ya uandaaji.

Zaidi amesema shahuku, kiu, ndoto na malengo yake ni kufika kimataifa zaidi na kutwa tuzo kubwa za muziki duniani.

“Kwa zaidi ya miaka minne bila kutoa Album, leo hii siwezi acha kumshukuru Jehova kwa kunipa kibali cha kufanya Album hii ya maisha yangu. Album inaitwa HARARAT ina nyimbo 25 na ndio album yangu yenye nyimbo nyingi kuliko zote nimewahi fanya” – ameeleza Shusho akitambulisha orodha ya nyimbo toka kwenye album yake.

Aidha, kwenye ujumbe wake mrefu, Christina Shusho amewaambia mashabiki waendelee kusalia kwenye kurasa zake kwani hivi karibuni atatangaza tarehe ya kufanyika kwa uzinduzi wa album hiyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke