You are currently viewing CHRISTINA SHUSHO AWEKA WAZI MATAMANIO YAKE YA KUSHINDA TUZO ZA BET

CHRISTINA SHUSHO AWEKA WAZI MATAMANIO YAKE YA KUSHINDA TUZO ZA BET

Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka Tanzania, Christina Shusho amesema kwamba yupo tayari na anajiandaa kwa tuzo za BET.

Akizungumza katika mahojiano na Presenter Ali, Shusho amesema kwamba kwa sasa tayari ameshashinda tuzo nyingi za ndani ya Tanzania na hata ukanda wa Afrika Mashariki ila kwa sasa anaazimia kuwania tuzo za kimataifa kama BET.

Aidha msanii huyo amesema kwamba kwa sasa analenga zaidi kuwashirikisha wasanii kutoka taifa la Congo katika kazi zake, ili kusukuma muziki wake nje ya Tanzania.

Hata hivyo Shusho amedokeza kwamba kwa sasa anaandaa albamu yake na maandalizi yake yanaelekea kukamilika, huku akisema kwamba mashabiki wake watarajie kazi nzuri na tofauti kutoka kwa album hiyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke