Mwimbaji nyota wa RnB kutoka Marekani Ciara amelibariki jarida la Ebony toleo la mwezi, Septemba ambapo amefunguka mambo kibao kuhusu muziki, maisha na mengine mengi.
Kubwa zaidi ambalo mrembo huyo amelizungumzia ni kuhusu ujio wa album yake mpya ikiwa ni baada ya miaka 3 alipoachia, Beauty Marks.
Ciara amesema mategemeo yake ni dunia nzima icheze kwa sababu ngoma zilizopo kwenye Album hiyo zina ‘energy’ ya kutosha.
Tayari ametanguliza wimbo wa kwanza kutoka kwenye album hiyo “Jump” ambao ulitoka mwezi Julai mwaka huu.