Msanii nyota nchini Uganda Cindy Sanyu amefunguka sababu za kususia show yake nchini Dubai wikiendi iliyopita.
Katika mahojiano yake Cindy amesema promota wa show hiyo aliingiwa na jeuri baada ya kushindwa kukamilisha malipo yake kabla ya kuingia jukwani kutumbuiza, jambo ambalo anadai lilimfanya kukataa kufanya performance yake.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Boom Party” ametoa changamoto kwa mapromota kuhakikisha wana pesa za kutosha kabla ya kuwapa wasanii mialiko ya kutumbuiza kwa show zao kwa sio kitendo cha kingwana kwa msanii kutumbuiza bila ys kulipwa haki yake.
Hata hivyo amewaomba radhi mashabiki zake wa Dubai msamaha kwa kutotokea kwenye show yake kutokana mgogoro uliobuka kati yake na promota wa onesho hilo.