Mwanamuziki kutoka Uganda Cindy Sanyu amewajibu baadhi ya watu wanaodai kuwa anawania urais wa chama cha wanamuziki nchini humo kwa ajili ya kupata pesa.
Katika kikao na wanahabari Cindy amesema ana utajiri mkubwa ambao aliupata kipindi anafanya kazi na makampuni mbali mbali.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Local Man” amesema lengo lake kuwania urais wa chama cha uma ni kuboresha tasnia ya muziki kwa faida ya vizazi vijavyo.
Hata hivyo amesema hajawahi pokea mshahara wowote tangu akuwe rais wa chama cha wanamuziki nchini Uganda.