Staa wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu ametangaza rasmi kurejea kwenye majukumu yake kama rais wa chama cha wanamuziki nchini humo baada ya kuchukua mapumziko mafupi.
Kupitia ukurasa wake amepost picha akiwa katika afisi za chama cha wasanii nchini uganda UMA huku akidokeza kuwa yupo tayari kwa ajili ya kuwasimamia wasanii na pia kuweka mikakati ya kuandaa uchaguzi wa chama hicho mwaka huu.
Kauli ya Cindy imekuja mara baada ya kukamilisha likizo aliyochukua kwa ajili kumlea mtoto wake aliyepata mwaka huu na mume wake Joel Atiku.
Utakumbukwa kabla miezi miwilli kabla ya kujifungua Cindy Sanyu aliruhusiwa kuchukua likizo fupi kama rais wa chama cha wasanii nchini uganda jambo ambalo lilimpelekea kusitisha kufanya shows kama njia ya kujiandaa kumpokea mtoto wake.