You are currently viewing CINDY SANYU AWACHANA WASANII WALIOTIA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA MUUNGANO WA WANAMUZIKI UGANDA

CINDY SANYU AWACHANA WASANII WALIOTIA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA MUUNGANO WA WANAMUZIKI UGANDA

Nyota wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu amewatolea uvivu wasanii ambao wametia nia ya kugombea wadhfa wa urais wa muungano wa wanamuziki nchini humo kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Cindy ambaye kwa sasa ni rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda amesema wasanii hao hawana vigezo vya kuongoza muungano huo na badala yake wamuachie nafasi akamilishe baadhi ya miradi ambayo alianzisha akiwa afisini kwa manufaa ya wanamuziki wote.

Kauli ya Cindy imekuja mara baada ya kuchukua na kujaza fomu ya kumuidhinisha kugombea tena wadhfa wa urais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda mapema wiki hii.

Utakumbuka wasanii kama Daddy Andre na King Saha wametangaza kuwania urais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda na sasa watachuana na cindy sanyu ambaye pia ametia nia ya kutetea wadhfa wake kwa mara ya pili.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke