You are currently viewing CLEVER J AFUNGUKA KUNYANYASWA NA PALLASO PAMOJA NA CHAMELEONE

CLEVER J AFUNGUKA KUNYANYASWA NA PALLASO PAMOJA NA CHAMELEONE

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka nchini Uganda Clever J ameonekana kukerwa na hatua ya Pallaso pamoja na Chameleone kushindwa kumlipa pesa zake licha ya kutumbuiza kwenye shows zao.

Katika mahojiano yake hivi karibuni CleverJ ameamua kutoa ya moyoni kwa kusema kwamba licha kutokea kwenye shoo sita za wawili hao hajapokea malipo yeyote. kwao.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Manzi Wanani” ametoa changamoto kwa Chameleone pamoja na mdogo wake Pallaso wamlipe haki yake akisema itakuwa ni jambo la aibu kwake kuanza kuwa omba omba ikizingatiwa kuwa watu wamekuwa wakimuona akitumbuiza kwenye shows mbali mbali.

Licha ya Clever J kuibua madai hayo Pallaso na Chameleone hawajatoa tamko lolote kuhusu tuhuma zilizoibuliwa na msanii huyo ila ni jambo la kusubiriwa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke