Msanii kutoka nchini Uganda Clever J hatomsamehe Jose Chameleone kwa kumpa ahadi ya uongo. Kipindi cha nyuma, Chameleone aliahidi kufanya wimbo wa pamoja na Clever J lakini hakufanikisha suala hilo.
Kulingana na Clever J, aliingia studio na Chameleone lakini bosi huyo wa Leone Island alitumia muda mchache tu kwenye kipasa sauti, na kisha akaondoka huku akiacha wimbo wao ukiwa umerekodiwa nusu.
Clever J anasema licha ya mashabiki kuendelea kushinikiza collabo kati yake na Chameleone hitmaker huyo wa “Manzi wa Nani” amedai kwamba hatofuatilia tena suala hilo.
Wimbo kati ya wawili hao ulipaswa kumtambulisha Clever J kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda kwa mara nyingine baada ya ukimya wa muda mrefu.