You are currently viewing CLEVER J: KIBURI IMENIPONZA KISANAA

CLEVER J: KIBURI IMENIPONZA KISANAA

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka nchini Uganda Clever J amekiri kuwa kitendo chake cha kutokubali kusimamiwa kikazi ndio imemponza kisanaa kwa miaka mingi.

Katika mahojiano yake ya hivi karibu hitmaker huyo wa ngoma ya “Manzi wa Nani” amesema hawezi stawi katika mazingira ya kupewa masharti ikizingatiwa kwamba hapendi kuwa chini ya shinikizo.

“Niliwaambia nyie kwamba mimi ni mtu mgumu sana. Sasa nataka kufanya mambo nipendavyo bila kuomba ruhusa,” alisema Clever

Utakumbuka Clever J alipata uongozi mpya miaka kadhaa iliyopita kwa ajili ya kuufuafua muziki wake lakini mwanamuziki huyo aligura uongozi wake huo na kuanza kufanya shughuli zake kama msanii wa kujitegemea.

Clever J alipata umaarufu kwenye muziki Afrika Mashariki mwaka wa 2007 kupitia wimbo wake uitwao “Manzi wa Nani” na alianza shughuli zake za kimuziki katika lebo ya muziki ya Leone Island inayomilikiwa na Jose Chameleone kabla ya kuondoka na kuhamua kuwa msanii wa kujitegemea.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke