You are currently viewing COLONEL MUSTAFA ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA.

COLONEL MUSTAFA ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA.

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Colonel Mustafa amerejea rasmi kwenye tasnia ya muziki baada ya ukimya wa miaka mitano.

Rapa huyo mwenye Asili ya Tanzania na Kenya amefichua kuwa yupo mbioni kuachia album yake mpya na tayari ameshaachia wimbo wake wa kwanza kutoka kwenye album hiyo iitwayo  Maloko ambao ameufanya na Prodyuza   Motif Di Don.

Akizungumza na NIAJE NIAJE rapa huyo amefunguka sababu za kuandika nyimbo zake mwenyewe kwa kusema kwamba huwa anajisikia mwenye faraja anapojiandikia nyimbo kwa sababu huwa anajieleza vizuri kupitia ubunifu wake binafsi.

“When someone else writes a songs for me, they don’t do as well as they do when I write them myself and they don’t get to express my thoughts fully. They will only write what is fit for them,” he says.

Hitmaker huyo wa Hey Baby amedokeza mpango wa kufanya remix ya wimbo wake Lenga Stress na wasanii wapya kwenye game kwani anaamini kizazi cha sasa kina uwezo mkubwa wa kumtoa sehemu na kupeleka kwingine kwenye muziki wake.

Utakumbuka Colonel Mustafa alitamba sana kipindi cha nyuma na nyimbo zake kali kama Monalisa, Adhiambo C, Mtaani dot com, Kinyau nyau na nyingine kibao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke