Msanii mwenye utata nchini Colonel Mustafa kwa mara nyingine amedai kuwa aliyekuwa mpenzi wake Noti Flow alimuibia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram.
Hitmaker huyo wa ngoma ya ‘Hey Baby’ amedai noti flow alichukua akaunti yake ya Instagram kwa njia ya mabavu kipindi wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Akizungumza kwenye the Trend ya NTV Mustafa amefichua kuwa masaibu yake yalianza wakati alitumia simu ya Noti Flow kuingia kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu alikuwa amepoteza simu yake.
Kulingana Mustafa Noti Flow alichukua maamuzi ya kubadilisha kila kitu kwenye ukurasa wake wa instagram bila ridhaa yake na akaanza kuchapisha vitu vyake binafsi jambo lilompelekea kufungua akaunti nyingine.
“She stole my Instagram account. Nililog in kwa simu yake, at that time I had lost my phone for like 2 to 3 weeks, so she wanted to post something aka change email address and everything so akaanza kupost vitu zengine zenye hazinihusu so nikaona hapa tu nikuchorea,” Amesema.
“She did not return the account, she took it, she changed it to her fan page so I had to find another one.” Ameongeza
Mustafa amesema kitendo cha kuachana na noti flow iliathiri maisha yake kiasi cha kuwafanya wasanii aliokuwa anafanya nao muziki kumpita kisanaa.
“I was not in peace…yaani ilifika point nikaona inanirudisha nyuma instead ya kuenda mbele…ata watu nilikuwa nao niliona wananipita,” amesema Mustafa.
Hata hivyo ameongeza kuwa yeye na noti flow sio marafiki kwa sasa na hajazungumza nae kwa muda mrefu.