Msanii mkongwe kwenye muziki wa Kenya Colonel Mustafa anazidi kufunguka tusiyoyajua kuhusu lebo yake ya zamani ya Ogopa Deejays.
Katika mahojiano yake hivi karibuni amesema karibu maamuzi magumu ya kuacha muziki baada ya lebo hiyo kuchukua umiliki wa nyimbo zake zote alizowahi kufanya kipindi cha nyuma.
Hitmaker huyo wa Katika amesema kitendo hicho kilimuingiza kwenye msongo wa mawazo kutokana na kutofaidi na mirahaba ya nyimbo zake.
Lakini pia amemchana dj mkongwe DJ Piye kwa kumbania kucheza nyimbo zake kwenye kipindi cha the beat ambapo ameanda mbali zaidi na kumtaja prezzo kuwa moja kati ya watu walioua muziki wa kenya kutokana na yeye kutengeneza matabaka miongoni mwa wasnii wa kenya.
Hata hivyo amekiri kuwahi kuingia kwenye ugomvi na msanii mwenzake Prezzo kwa sababu ya wanawake ambapo amemuomba radhi msanii huyo kutokana na kile kilichotokea kati ya yao.
Mustafa kwa sasa yupo mbioni kuachia album yake mpya ambayo hajaweka wazi idadi ya ngoma wala tarehe ya kuingia rasmi sokoni ila ni jambo la kusubiriwa.