Klabu ya Tottenham imemtangaza Antonio Conte kuwa kocha wake mpya akichukua nafasi ya Nuno Espirito Santo aliyefukuzwa kazi Novemba mosi mwaka huu.
Kocha huyo wa zamani wa Klabu za Juventus, Chelsea na Inter Milan amesaini kandarasi ya miezi 18.
Kocha Nuno Espirito Santo amefungashiwa virago na Klabu hiyo ya Jijini London ikiwa ni miezi minne tangu alipoanza kuinoa timu hiyo.
Kocha huyo ameiongoza Spurs katika michezo 17, ameshinda michezo 8, kafungwa 7 na kutoka sare michezo 2 huku timu hiyo ikifunga magoli 21 na kufungwa 23.