You are currently viewing Corazon Kwamboka kushtaki duka la jumla nchini Uganda kwa kutumia picha zake bila idhini

Corazon Kwamboka kushtaki duka la jumla nchini Uganda kwa kutumia picha zake bila idhini

Sosholaiti  maarufu mtandaoni Corazon Kwamboka amedai kuwa atachukua hatua kali za kisheria dhidi ya duka la moja la jumla nchini Uganda ambalo lilitumia picha zake bila ridhaa yake.

Duka hilo lilitumia picha zake kwa matangazo na madhumuni ya kibiashara bila idhini yake hivyo kukiuka haki zake za faragha na umaarufu.

Taarifa hizo zilifikishwa kwake na mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii ambapo amesema amewasiliana na wakili wake kulifanyia kazi suala la kuufungulia kesi maduka hayo.

Corazon alijizolea umaarufu kwa mara ya kwanza baada ya picha zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, wakati akiwa bado katika shule ya sheria. Aliorodheshwa kama mmoja wa warembo wakali Zaidi nchini Kenya kutokana na muonekano wake wa kuvutia.

Kulingana naye, hakuwa na nia ya kuwa Sosholaiti lakini anashukuru Mungu kwa kuwa wakenya walimkubali jinsi alivyo kwa kauli moja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke