Rapper mkali kwa michano kutoka Tanzania country boy amefunguka namna lebo ya muziki ya Konde Gang ilivyobadilisha maisha yake na kuupa hadhi mziki wa Hip Hop nchini tanzania.
Kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni, rapa huyo amesema kuwa chini ya lebo hiyo imemuongezea thamani kama msanii na hata imepelekea hadhi ya muziki wa hiphop tanzania kupanda kwani mara nyingi wasanii wa Hip-hop huwa wanakosa nafasi ya kujiunga na lebo kubwa.
Kwenye lebo ya Konde Gang, Country boy ndiye msanii pekee anayefanya muziki wa Hip-hop na Kabla ya kuingia kwenye lebo hiyo, Rapa huyo alipita kwenye lebo kadhaa za muziki ikiwemo Rooftop Entertainment.