Rappa kutoka Tanzania Country Wizzy ameweka wazi mpango wake wa kuingia kwenye baishara ya mavazi ambapo amesema kabla ya mwaka huu kuisha atakuwa tayari ameshafungua duka lake la nguo.
Mkali huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake “You” ametambua kuwa kwa hatua aliyofikia, si muziki wake pekee unaouza, bali ni jina lake ndilo lenye thamani zaidi ya kitu chochote kwa sasa. Kwa mtaji wa jina lake na wafuasi wake, anaweza kutengeneza fedha nyingi zaidi kupitia biashara.
Kwenye posti yake aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Country Wizzy pia amewataka mashabiki wake wampe jina la duka hilo huku komenti zikiwa nyingi na zote zikipendekeza duka lake kuitwa Country Boy.