Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo jana Disemba 14, 2022 alikuwa katika uwanja wa Real Madrid na kufanya mazoezi maalum chini kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti.
Cristiano alikuwa pamoja na mwanawe na aliomba ruhusa ya kufanya mazoezi katika vituo vya Madrid baada ya Timu yake Kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia.
Rais wa Real Madrid Florentino Perez na Timu yake walikubali ombi la Ronaldo bila kipingamizi kutoka na uhusiano mzuri kati yao.
Ronaldo alifanya mazoezi ya peke yake tofauti na kikosi cha kwanza, cha Carlo Ancelotti.
Kwa sasa hakuna mazungumzo yanayoendelea ya kumrejesha Real Madrid.