You are currently viewing “CRYPTO” WALLET MPYA YA FACEBOOK YAANZA KUFANYA KAZI

“CRYPTO” WALLET MPYA YA FACEBOOK YAANZA KUFANYA KAZI

Baada ya Facebook kusumbuliwa na fedha ya kidigitali ya Libra, iliamua kuipa jina la “Diem” na kuwekeza katika kutengeneza Wallet ya Novi ambayo itatumika kutuma na kupokea fedha na itaunganishwa na crypto, metaverse, mfumo wa matangazo, na apps za Instagram, Facebook na WhatsApp ambapo watumiaji wataweza kutuma na kupokea fedha bure kwa urahisi. Kwa sasa Wallet (pochi ya kidigitali) ina crypto (stable coin) ya Paxos Dollar ambayo ina thamani sawa na Dola.

Mkuu wa Idara ya Facebook inayosimamia Novi Wallet, David Marcus amesema kuna zaidi ya watu Bilioni 1.7 ambao hawana akaunti za kibenki na zaidi ya watu Bilioni 1 hawafurahishwi na mfumo wa mabenki hasa katika makato ya kutuma na kupokea fedha.

Facebook imeanza kutoa wallet yake ya Novi kuanza kutumika kwa wakazi wa Marekani na Guatemala. Novi Wallet ni wallet ya Facebook ambayo itakuwa haina makato katika kutuma na kupokea fedha. Ni salama,haikusanyi data na Facebook imejaribu kuweka umakini ili kuepusha sifa mbaya katika kusimamia mfumo huo wa kifedha.

Wallet hiyo inatumia coin ya Pax Dollar (USDP) na wiki hii imeshirikiana na Coinbase kuwezesha watumiaji kununua na kuuza Pax Coin kwa kutumia wallet hizo mbili. Wallet ya Novi itakuwa haina makato katika kutuma fedha, ni salama  na inatumia mifumo mikubwa ya kuthibiti usalama na urahisi kwa watumiaji. Facebook inajaribu kuifanya iwe “Wallet ya mitandao ya kijamii”.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke