Aliyekuwa msanii wa Sol Generation Crystal Asige amechapishwa rasmi kwenye gazeti la serikali kama seneta mteule atakayewakilisha watu wenye changamoto ya ulemavu bungeni.
Katika notisi iliyotolewa na tume ya IEBC Septemba 7, jina la Asige limetajwa kwenye orodha ya viongozi walioteuliwa kujiunga na bunge la kitaifa pamoja na seneti.
Mwimbaji huyo ameteuliwa kwa tiketi ya chama cha ODM huku UDA ikimteua George Mungai kama mwakilishi wa kiume wa watu wenye changamoto ya ulemavu.