You are currently viewing DABABY KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUMPIGA NGUMI NA KUMG’OA MTU JINO

DABABY KUFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUMPIGA NGUMI NA KUMG’OA MTU JINO

Rapa kutoka Marekani DaBaby anakabiliwa na mashtaka ya jinai kwa kuhusishwa na kesi ya kumpiga mwanamume mmoja anayedaiwa kujaribu kuwazuia wasaidizi wa rapa huyo kufanya video ya muziki katika eneo lake

Rapa huyo amefunguliwa mashtaka ya uhalifu na ofisi ya mwanasheria wa wilaya huko Los Angeles kufuatia tukio lililotokea mapema mwezi Desemba mwaka jana 2021 ambalo linadaiwa kumsababishia majeraha mabaya Gary Pagar ambaye ni mmiliki wa jumba hilo walilopangisha.

Pagar aliwasilisha kesi kwa vyombo vya usalama mapema Februari, akidai alishambuliwa kwa kutekeleza sheria za msingi za kukodisha nyumba yake ambayo rapa Dababy alikodishiwa kwa ajili ya mapumziko mafupi ya likizo.

Miongonia mwa masharti aliyotoa baba mwenye nyumba huyo ni kuwa DaBaby hakuruhusiwa kuwa na wageni zaidi ya 12 kwa wakati mmoja ndani ya jengo hilo la kifahari

Baada ya kipindi cha wiki mbili Pagar anasema alibaini kwamba kulikuwa na zaidi ya watu 12, jambo lililompelekea kuilalamikia timu ya DaBaby kwa kukiuka makubaliano yao ya awali.

Ilipofika Desemba 2, anasema alitembelea nyumba hiyo yeye mwenyewe na kugundua kwamba walikuwa wakirekodi video ya muziki na kikundi kizima cha filamu na idadi kubwa ya watu ambao anakadiria kuwa walifika zaidi ya 40, jambo lililomfanya ajaribu kuwazuia kuendelea na shughuli hiyo kwa kuwa tayari wamevunja utaratibu.

Na hapo ndipo anapodai kuwa alianza kushambuliwa na mmoja wa wafanyakazi wa rapa DaBaby, sehemu ambayo kwa bahati ilinaswa kwenye video,Pagar anadai kuwa baada ya muda mfupi DaBaby alimuamuru mfanyakazi wake huyo kuacha kumshambulia lakini aliendelea kumpiga ngumi usoni hadi kumsababishia jino lake kung’oka.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke