You are currently viewing DABABY KWENYE HEADLINES BAADA YA KUZICHAPA NA MSANII MWENZAKE

DABABY KWENYE HEADLINES BAADA YA KUZICHAPA NA MSANII MWENZAKE

Rapa asiyeishiwa na vituko kutoka nchini Marekani, Da Baby, kwa mara nyingine ameingia kwenye headlines mtandaoni baada ya kuzichapa kavukavu na msanii mwenzake.

Da Baby amezichapa na msanii ambaye wapo naye lebo moja, Wisdom wakiwa ‘backstage’ wakati wa tamasha la Spring Jam 2022 lililofanyika katika Ukumbi wa Colonial Life Arena, Columbus, South Calorina usiku wa Ijumaa.

Tukio hilo linakuja wiki mbili tangu msanii huyo alipofanya tukio lingine la kumpiga risasi ya mguu mtu aliyevamia makazi yake, baada ya kutokea hali ya kutoelewana kati yao.

Siku kadhaa nyuma, Da Baby alifanya kituko kingine baada ya kunaswa na kamera za CCTV akitaka kumbusu shabiki wake wa kike kwa lazima huku akionesha kuzidiwa na kilevi.

Hata hivyo haijafahamika bado nini kinamsumbua Hitmaker huyo wa “Rock Star” mpaka kuwa na matukio ya ajabu mfululizo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke