Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini daddy owen amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa anatafuta mwanamke wa kuingia naye kwenye ndoa ikiwa ni siku chache zimepita toka alipoweka wazi vigezo anavyohitaji kutoka kwa mwanamke wà ndoto yake.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Daddy Owen amesema kauli yake ilinukuliwa vibaya na walimwengu huku akisema kama kweli angekuwa anatafuta mke angefanya hivyo bila kuwafahamishw watu ikingatiwa kuwa yeye bado ni mwanaume rijali ambaye ana uwezo mkubwa wa kutongoza mwanamke.
Hitmaker huyo wa Vanity amewataka walimwengu kuacha kueneza propaganda mtandaoni kuwa anatafuta mke wa kuoa na badala yake wamuunge mkono kwenye muziki wake kwani ikitokea kuwa ameingia kwenye mahusiano ataweka wazi kwa mashabiki zake.
Kauli ya Daddy Owen imekuja mara baada ya kuzua gumzo mtandaoni kuwa anatafuta mwanamke ambaye anatoka mashinani, na mcha mungu ili aweze kuingia naye kwenye ndoa ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka wadada ambao wanatamani kutokana nae kimapenzi kutuma maombi kupitia mitandao yake ya kijamii.