You are currently viewing DADDY ANDRE AKANA KUTOKA KIMAPENZI NA VIDEO VIXEN BOBO SHAN

DADDY ANDRE AKANA KUTOKA KIMAPENZI NA VIDEO VIXEN BOBO SHAN

Msanii na prodyuza wa muziki kutoka nchini Uganda Daddy Andre amekanusha uvumi unaotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na video vixen Bobo Shan ambaye anadaiwa ana uja uzito wake .

Akiwa kwenye moja ya Interview Daddy Andrea  amesema uvumi huo hauna ukweli wowote ikizingatiwa kuwa hamfahamu kabisa mrembo huyo.

Hitmaker “Omwana Bandi” amesema ikutokea yupo kwenye mahusiano mapya atatambulisha mpenzi wake kwa umma kwani hapendi kuficha mahusiano yake.

Kauli Daddy Andre imekuja mara ya kudaiwa prodyuza yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na video vixen Bobo Shan ambaye watumiaji wa mitando ya kijamii walienda mbali zaidi na kuhoji kwamba ana uja uzito wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke